• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Project and Program
    • RISE - MAY- 2021
    • TeRMIS
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Barabara
      • Sehemu ya Barabara Vijijini
      • Sehemu ya Barabara Mijini
    • Kurugenzi ya Mipango na Miundombinu
      • Sehemu ya Usalama Barabarani
      • Sehemu ya Mipango na Miundombinu ya Barabara
    • Kurugenzi ya Huduma Saidizi
      • Sehemu ya Rasilimali Watu na Utawala
      • Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini
    • Kitengo cha Uhasibu
    • Kitengo cha Tafiti na Udhibiti Ubora
    • Kitengo cha Teknlojia ya Habari na Takwimu
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Ununuzi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
    • Kitengo cha Mazingira na Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Mameneja wa Mikoa
    • Mameneja wa Wilaya

BODI YA USHAURI YA TARURA YARIDHISHWA NA UJENZI WA BARABARA KILOLO

Posted on: July 12th, 2022

BODI YA USHAURI YA TARURA YARIDHISHWA NA UJENZI WA BARABARA KILOLO

Na. Geofrey Kazaula, Iringa.

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Florian Kabaka wamekagua ujenzi wa Barabara ya Kidabaga - Boma la Ng’ombe wilayani  Kilolo mkoani Iringa na kuridhishwa na ujenzi.

Akiwa Wilayani Kilolo katika ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Barabara za “Agri-Connect", Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Florian Kabaka ameeleza  kuridhishwa  na ujenzi wa  Barabara ya Kidabaga-Boma la Ng'ombe iliyojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa km 18.3.

Mhandisi Kabaka amebainisha kuwa lengo la Serikali kupitia TARURA ni kuhakikisha barabara za vijijini zinaboreshwa  ili kuwezesha wananchi kusafirisha mazao yao kwa urahisi na kukuza uchumi wao.

''Tumekagua mradi huu hapa Kilolo na kujionea kazi nzuri iliyofanywa na TARURA, mradi umekamilika na sasa wananchi watatumia muda mfupi kusafiri na kusafirisha mazao yao,” alisema Mhandisi Kabaka.

Kwaupande wake Makamu Mweyekiti wa  Bodi hiyo, Bibi Julieth Magambo amesema kuwa uchumi wa wananchi unategemea Barabara na hivyo Serikali itaendelea kuboresha barabara za vijijini ili wananchi waweze kuzifikia huduma za kijamii kwa urahisi na kuboresha uchumi wao.

Aidha alieleza kuwa ni jukumu la Bodi kuzisimamia barabara hizo na kumuunga mkono Rais Samia ambaye ameamua kwa dhati kuhakikisha kuwa barabara za Vijijini zinafunguka na kuwafikia wananchi ili ziwaunganishe na miji na kurahisisha usafiri na usafirishaji.

Naye Mkurugenzi wa Barabara TARURA, Mhandisi Venant Komba amesema kuwa  TARURA inaendelea na ujenzi wa Barabara ikiwa ni pamoja na kufungua barabara mpya ili kuwezesha wananchi kuyafikia maeneo haliyokuwa hayafikiki.

Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa Mikoa miwili inayotekeleza miradi ya ujenzi wa barabara za Lami “ Agri-Connect “ chini ya ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya.

Mradi huu unalenga kuwasaidia Wakulima vijijini kuimarisha Mnyororo wa thamani ya Mazao yao hasa mazao ya Chai,Kahawa,Mbogamboga na mazao mengine yanayohitaji kusafirishwa kwa haraka toka Mashambani hadi Viwandani na Sokoni.

Matangazo

  • INVITATION FOR TENDERS - DODOMA June 08, 2022
  • TANGAZO LA KAZI -KAGERA April 21, 2022
  • CALL FOR INTERVIEW - MTWARA January 17, 2022
  • CALL FOR AN INTERVIEW - MWANZA December 23, 2021
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TARURA YASAINI MIKATABA YA MABILIONI KUIMARISHA MTANDAO WA BARABARA VIJIJINI NA MIJINI

    August 14, 2022
  • MAAGIZO 10 YA RAIS SAMIA KWA TAMISEMI NA TARURA

    August 14, 2022
  • WANANCHI KILOSA WAFURAHIA UJENZI DARAJA LA BEREGA

    August 12, 2022
  • RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KM 40 MUFINDI, IRINGA

    August 11, 2022
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Barua pepe za Watumishi - TARURA
  • Mfumo wa Maegesho (TeRMIS)
  • Lipia Maegesho (TeRMIS)
  • Mfumo wa eMrejesho

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Instragram_tarura
  • twitter_tarura
  • Mfumo wa Maegesho (TeRMIS)
  • Mfumo wa eMrejesho

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),TARURA HOUSE GOVERNMENT CITY -MTUMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa