• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Miradi iliyo kamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyochini ya Ununuzi
    • Project and Program
    • RISE - DEC 2020
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Huduma na Uendeshaji
    • Kurugenzi ya Barabara za Vijijini
    • Kurugenzi ya Barabara za Mijini
    • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
    • Kitengo cha udhibiti Ubora na Utafiti
    • Sehemu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)
    • Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu
    • Sehemu ya Mipango
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri

MHE. JAFO ATOA NENO KWA BODI MPYA YA USHAURI YA TARURA

Posted on: May 30th, 2020

Na. Geofrey Kazaula na Bebi Kapenya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ameitaka Bodi mpya ya Ushauri ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kusaidia, kubuni na kupanga mikakati ya kuisaidia TARURA iweze kusimama imara na kuweza kusaidia wananchi.

Mhe. Jafo aliyasema hayo wakati akiizindua Bodi ya Kwanza ya Ushauri ya TARURA chini ya Mwenyekiti wake, Mhandisi Florian Kabaka katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la Mawaziri (Mkapa House) jijini Dodoma hivi karibuni.

“Nawapongeza wote kwa ujumla wenu kwa kupewa dhamana hii kwa niaba ya watanzania kuja kukisimamia chombo hiki muhimu ambacho ni hitaji kubwa sana la wananchi wote wa Tanzania. Ninyi ndio mnakwenda kuzindua Bodi ya Kwanza ya TARURA maana yake mna kazi kubwa ya kufanya ya kutengeneza msingi mzuri, hivyo basi, sina mashaka na Bodi hii na naamini itaenda kuweka misingi imara katika kipindi cha miaka yake mitatu (3)”, alisema.

Aidha, Mhe. Jafo amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff kuwa mkali na kuwachukulia hatua Waratibu wa TARURA wa Mikoa wazembe wanaosabisha kazi zisiende kama ilivyokusudiwa na kukwamisha utendaji kazi wa Wakala.

“Mtendaji Mkuu, pitia kamati zako zote za manunuzi za mikoa ambazo hazifanyi vizuri, ondoa undeni tena, hatuwezi kuwa na kamati ambazo fedha zinapelekwa, lakini kuna Waratibu ambao ni wazembe wanaochelewesha utekelezaji wa miradi na ukiomba taarifa haziji kwa wakati, aina ya kamati hii haina sifa ya kuendelea kuwepo”, alisema.

Pia, akizungumzia kuhusu rasilimali fedha kuhusu Wakala, Waziri Jafo alisema TARURA kwa kiwango kikubwa inategemea fedha kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara ambapo inapata asilimia 30 huku Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ikipata asilimia 70 na kuna kazi kubwa inafanyika ya kutafuta fedha kutoka vyanzo vingine ili TARURA iweze kuhudumia wananchi.

Kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa na Wakala, Mhe. Jafo alisema miaka mitatu sasa TARURA imejijengea heshima kwa wadau wakiwemo wabunge kutokana na kazi kubwa iliyofanyika.

“Niwapongeze watendaji kwa kazi nzuri, leo hii ukiwa pale bungeni, kila mbunge anashuhudia kazi nzuri ya weledi iliyofanywa na TARURA, changamoto ni bajeti ndogo lakini timu hii imefanya kazi licha ya changamoto ya upya na uchache wenu kwa kipindi chote hiki mmeweza kufanya kazi kubwa sana”, alisema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Joseph Nyamhanga alisema bodi hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha Wakala unafanya kazi vizuri licha ya kuwa na tatizo la ufinyu wa bajeti.

Alisema tayari wamewasilisha maombi ya kupata fedha za kuanzia kutoka Wizara ya Fedha na Mipango shilingi Bilioni 55.8 kwa ajili ya kuziboresha barabara zilizoharibika wakati wa mvua ambapo kwa mujibu wa tathmini iliyofanyika inahitajika shilingi bilioni 132 ili kurejesha miundombinu hiyo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi, Mhandisi Florian Kabaka amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kumteua kuongoza bodi hiyo ambayo ndio mara ya kwanza imeanzishwa na kuahidi kufanya kazi kwa uwezo wote kwa kushirikiana na wajumbe wa bodi pamoja na wafanyakazi ili kuhakikisha TARURA inakua zaidi ya ilivyo sasa katika kuwahudumia watanzania.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo, Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff alisema, Wakala huo uliundwa rasmi mwaka 2017 kwa lengo la kutoa matengenezo endelevu na gharama nafuu ili kusaidia maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii nchini.

Amehaidi kutoa ushirikiano kwa Bodi ili kuweza kuipeleka TARURA pale ambapo wananchi wana matarajio hasa kwa hizi mvua zilizonyesha na kuharibu miundombinu kwani Bodi itasaidia kufanya ushawishi ili kupata rasilimali za kutosha katika kutekeleza majukumu ya Wakala.

Wajumbe wanaounda Bodi mpya ya Ushauri ya TARURA ni Mhandisi Florian M. Kabaka (Mwenyekiti), Bi. Julieth S. Magambo (mjumbe), Mhandisi John A.F. Ngowi (mjumbe), Bw. Hussein A. Wandwi (mjumbe), Bw. Leo J. Ngowi (mjumbe), Bw. Ismail A. Manjoti (mjumbe) na Mhandisi Gilbert G. Mwoga (mjumbe).

Mwisho. 

 

Matangazo

  • INVITATION FOR LOGO DESIGN COMPETITION November 12, 2020
  • SHINDANO LA KUANDAA NEMBO (LOGO) YA TARURA-KISWAHILI November 12, 2020
  • WALIOITWA KWENYE USAILI KADA YA UDEREVA TARURA MKOA WA TANGA November 06, 2020
  • KUITWA KWENYE USAILI-KIGOMA October 30, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TARURA WAHIMIZWA KUONGEZA KASI YA UTENDAJI KAZI

    December 17, 2020
  • TARURA WILAYANI LIWALE YATEKELEZA MIRADI YA AHADI ZA VIONGOZI

    December 10, 2020
  • TARURA YAPONGEZWA UJENZI WA DARAJA LA KANKWALE MKOANI RUKWA

    December 08, 2020
  • BILLION 7.4 ZATUMIKA KUING’ARISHA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA

    December 07, 2020
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Tarura Barua pepe za Watumishi

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Instragram_tarura
  • twitter_tarura

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),TARURA HOUSE GOVERNMENT CITY -MTUMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa