• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
      • Bodi ya Ushauri
      • Uongozi wa Wakala
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Project and Program
    • RISE - MAY- 2021
    • TeRMIS
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Barabara
      • Sehemu ya Barabara Vijijini
      • Sehemu ya Barabara Mijini
    • Kurugenzi ya Mipango na Miundombinu
      • Sehemu ya Usalama Barabarani
      • Sehemu ya Mipango na Miundombinu ya Barabara
    • Kurugenzi ya Huduma Saidizi
      • Sehemu ya Rasilimali Watu na Utawala
      • Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini
    • Kitengo cha Uhasibu
    • Kitengo cha Tafiti na Udhibiti Ubora
    • Kitengo cha Teknlojia ya Habari na Takwimu
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Ununuzi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
    • Kitengo cha Mazingira na Maendeleo ya Jamii
    • Ofisi ya Mkoa
    • Ofisi ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Mameneja wa Mikoa
    • Mameneja wa Wilaya

TARURA DAR YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI BASHUNGWA

Posted on: January 21st, 2022

TARURA DAR YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI BASHUNGWA

Na. Mwandishi wetu

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam umeanza kutekeleza agizo la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Innocent Bashungwa ambaye aliagiza Mameneja wa TARURA kwenye Wilaya kushiriki vikao vya Mabaraza ya Madiwani na kujibu hoja zinazojitokeza katika masuala ya barabara.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Geofrey Mkinga ameeleza kuwa hivi karibuni wameanza  vikao vya kuwashirikisha viongozi wa Halmashauri hasa Madiwani kwenye maandalizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

“Tupo kwenye maandalizi ya bajeti ya mwaka 2022/2023 ambapo kama mnavyojua vikao vya Bunge vinatarajiwa kuanza mwezi wa 4, hivyo sisi tumeendelea kufanya vikao vile vya chini kuanzia ngazi ya Kata, Baraza la Madiwani pamoja na Bodi ya Barabara ya Mkoa ili kuhakikisha kwamba mapitio ya bajeti na mapendekezo yote ya vipaumbele vya barabara tunawashirikisha” alisema Mhandisi Mkinga.

Mhandisi Mkinga alisema hadi sasa wameshafanya vikao vya ushirikishwaji katika Wilaya ya Ilala, Kinondoni, Ubungo, Ilala na Kigamboni ambapo alieleza kuwa lengo ni kuwaonesha rasimu ya bajeti na wamefanya hivyo kwa sababu vyanzo vyao vya fedha ni vitatu ambavyo ni kutoka Serikali Kuu, Halmashauri pamoja na Wadau wa Maendeleo ikiwemo miradi ya DMDP ambayo hutokana na mikopo au ufadhili.

“Tunavyowashirikisha Waheshimiwa Madiwani wanaona uwezo wa Serikali katika kuhudumia bajeti kwa maana ya Serikali Kuu, lakini pia na wao wanapata wasaa wa kuona watachangia kiasi gani, tumefanya hivi kabla ya vikao vyao vya kibajeti havijaanza ili sasa waone wanatupangia nini, kwa sababu barabara nyingi zipo kwao", alisema Mhandisi Mkinga.

Mhandisi Mkinga alieleza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una mtandao wa barabara ambao zaidi ya asilimia 50 una hali mbaya huku asilimia nyingine 50 ukiwa na hali nzuri na wastani hivyo wanahitaji ushirikiano mkubwa wa viongozi hao wa Halmashauri kwa maana ya Madiwani ambao ndiyo wenye fedha na pia kuwasaidia kujua barabara gani ni muhimu ambazo zinapaswa kupewa kipaumbele katika matengenezo.

Akizungumzia kuhusu mfumo wa ukusanyaji mapato ya maegesho ya vyombo vya moto (magari) kwa njia ya kielekroniki, alisema kuwa mfumo ulipoanza kutumika kwa mara ya kwanza mwezi Septemba mkoani Dar es Salaam kabla ya kusitishwa mwezi Oktoba 2021 kulikuwepo na changamoto mbalimbali zilizojitokeza ambapo changamoto hizo zilitatuliwa na mfumo ulianza kutumika tena mwezi Desemba 2021 na wananchi wanaendelea kuutumia mfumo huo.

Alieleza kuwa moja wapo ya changamoto iliyojitokeza ilikuwa ni elimu kwani wananchi wengi hawakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya mfumo huo na kusema kuwa kwa sasa elimu inaendelea kutolewa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Desemba 2021 mpaka mwezi Februari 2022 kabla ya kuanza kufungulia faini na kusisitiza wale wote wenye madeni kulipa madeni yao ili kuepuka usumbufu. Kwa sasa mtumiaji wa maegesho anapaswa kulipia maegesho ndani ya Siku 14 kushindwa kulipia ndani ya muda huo atakutana na faini ya Shilingi 10,000 na gharama ya maegesho ni Shilingi 500 kwa Saa na Shilingi 2,500 kwa Siku.

Aidha Mhandisi Mkinga alieleza kuwa muda wa kulipia maegesho ni kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa Siku za Wiki na kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 7 mchana siku ya Jumamosi, Siku ya Jumapili na Sikukuu hawatozi maegesho na kusisitiza wananchi waendelee kulipia madeni yao pale wanapotumia maegesho kupitia mitandao ya simu, benki ya NMB na CRDB au kwa Mawakala wa Huduma za fedha.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI -KAGERA April 21, 2022
  • CALL FOR INTERVIEW - MTWARA January 17, 2022
  • CALL FOR AN INTERVIEW - MWANZA December 23, 2021
  • TANGAZO LA KAZI -MWANZA December 10, 2021
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ZIARA YA MTENDAJI MKUU TARURA YALETA FARAJA KWA WANANCHI - KASEKE

    May 19, 2022
  • TARURA TANGANYIKA WAPEWA SIKU 30 KUKAMILISHA UKARABATI DARAJA LA IFUME

    May 18, 2022
  • WATUMISHI TARURA WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    May 16, 2022
  • BODI YA USHAURI TARURA YAFANYA UKAGUZI UJENZI WA BARABARA KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA

    April 29, 2022
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Barua pepe za Watumishi - TARURA
  • Mfumo wa Maegesho (TeRMIS)
  • Lipia Maegesho (TeRMIS)
  • Mfumo wa eMrejesho

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Instragram_tarura
  • twitter_tarura
  • Mfumo wa Maegesho (TeRMIS)
  • Mfumo wa eMrejesho

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),TARURA HOUSE GOVERNMENT CITY -MTUMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa