• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Project and Program
    • RISE - MAY- 2021
    • TeRMIS
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Barabara
      • Sehemu ya Barabara Vijijini
      • Sehemu ya Barabara Mijini
    • Kurugenzi ya Mipango na Miundombinu
      • Sehemu ya Usalama Barabarani
      • Sehemu ya Mipango na Miundombinu ya Barabara
    • Kurugenzi ya Huduma Saidizi
      • Sehemu ya Rasilimali Watu na Utawala
      • Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini
    • Kitengo cha Uhasibu
    • Kitengo cha Tafiti na Udhibiti Ubora
    • Kitengo cha Teknlojia ya Habari na Takwimu
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Ununuzi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
    • Kitengo cha Mazingira na Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Mameneja wa Mikoa
    • Mameneja wa Wilaya

TARURA IMEUNGA MKONO AGIZO LA SERIKALI

Posted on: April 24th, 2019

TARURA IMEUNGA MKONO AGIZO LA SERIKALI, IMEKUJA NA MFUMO WA TARURA ePARKING UNAOTAJWA KUWA MWAROBAINI WA MALALAMIKO, SASA MALIPO NI KIGANJANI MWAKO

Na Erick Mwanakulya.

MWAKA jana serikali ilitoa maagizo kwa taasisi za serikali kuhakikisha ifikapo juni mwaka huu ziwe zimeshajiunga kwenye mfumo wa malipo wa serikali kwa njia za kielektroniki (GePG).

Lengo la kujiunga katika mfumo huo ni kutimiza azma yake ya kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma.

Katika kutekeleza hilo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), umezindua mfumo wa kukusanya ushuru wa maegesho wa vyombo vya moto kwa njia ya kielektroniki (TARURA e-parking) mkoani Mwanza ambao unatumia mfumo wa GePG ili kutimiza matakwa ya sheria ya fedha za umma sura ya 348.

Mfumo huo unatajwa kuondoa hofu na kujibu maswali yaliyokuwepo awali kwamba je pesa wanazotoa kweli zinafika kunakohusika?

Awali ushuru ulikuwa unatozwa na halmashauri na baadae jukumu hilo likahamishiwa TARURA.

TARURA inatoza ushuru kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria Na. 8.1 (vi) “Parking Fee on Road Reserve” ambapo mwanzoni walikuwa wanatumia utaratibu wa kukusanya ushuru kwa njia ya vitabu vya mkono na baadae serikali ikaleta mashine za POS (Point of Sale).

Kwa sasa TARURA imeona ije na mfumo wa TARURA e-parking utakaowezesha mwananchi kulipa pesa moja kwa moja kwenye akaunti ya serikali.

Kabla ya kuanza kwa mfumo huo wakala huo umewaandaa wadau mbalimbali kwa kuwapa elimu ili waujue na kuuelewa kutumia mfumo.

Akizungumza na Makala hii mratibu wa TARURA mkoa wa Mwanza mhandisi Koyoya Fuko anasema mfumo huo unaanza kutumika mei 2 mkoani humo katika jiji la Mwanza na halmashauri ya manispaa ya Ilemela kwa majaribio na baadae utaenda nchi nzima dhamira ikiwa ni kumfanya kila mwananchi alipe ushuru wa maegesho kwa hiyari.

Faida nyingi zinatajwa kuwepo katika matumizi ya mfumo huo ikiwemo kulinda na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya serikali yatakayosaidia kuboresha miundombinu ya barabara nchini.

“Mfumo wa zamani uliokuwa unatumika ulikuwa unatoa mianya kwa mtu asiye muaminifu kuweza kufanya chochote kwa kushirikiana na mteja wetu na hivyo kuikosesha serikali mapato, anaweza akakusanya ushuru asitoe risiti na hela ikaiishia mfukoni mwake lakini kwa mfumo huu hilo halitaweza kufanyika,

Mfano mdogo tu ni huu, tumefanya tathmini kwa kipindi cha wiki mbili katika jiji la Mwanza na manispaa ya halmashauri ya Ilemela tumegundua idadi ya magari yanayopaki na kulipa ushuru ni nusu tu ya magari yote yanayopaki hivyo upotevu wa mapato upo,”anasema Fuko.

Aidha anasema zamani usalama wa watoza ushuru pia haukuwa wa uhakika kwa kuwa mtu yoyote angeweza kuwakaba na kuwanyang’anya hela walizokusanya lakini kwa sasa hela itakuwa haishikwi mikononi bali inaingia kwenye akaunti ya serikali moja kwa moja.

Fuko anataja faida nyingine kuwa ni kuimarisha ulinzi,kuondoa bugudha iliyokuwepo awali kutokana na kuwa rafiki,utapunguza kero za madai ya ushuru kwa watumiaji wa maengesho.

“Kwa mfumo huu mpya mtu anaweza kulipa muda wowote kwa siku nzima ili mradi isizidi siku husika ili asikutane na faini ya shilingi 40,000 endapo atapitisha bila kulipa,sasa hivi ushuru unatakiwa kulipa hapo hapo lakini kwa mfumo huu utaweza kulipa hata ukiwa nyumbani kwa kutumia simu za mkononi,mawakala au benki,”alisema Fuko.

Pia mfumo utasaidia kuupanga mji vizuri kwa kuwa na sehemu nyingi za maegesho na kuboresha mipango ya barabara ili kupunguza changamoto za maegesho.

“Kupitia mfumo huo tutajua idadi ya magari yanayoingia mjini,sisi wahandisi tunatakiwa tujue ili kuandaa mipango mizuri ya kuweka maegesho,”anasema mratibu huyo.

Anasema mipango iliyopo kwa sasa ni kutengeneza ramani ya eneo la maegesho ili kila mtu akifika ajue na wakitekeleza hili wataondoa ule utaratibu wa magari kufungwa cheni kwa kuegesha vibaya.

Swali moja kubwa ambalo lipo vichwani mwa watu wengi ni je kuanza kwa matumizi ya mfumo huo hakukatishi ajira za mawakala waliopo kwa sasa katika kukusanya ushuru?

Afisa Uhusiano na Mawasiliano kutoka TARURA Makao Makuu Mwansith Kitogo anasema kabla ya kuanza maandalizi ya utumiaji wa mfumo huo,TARURA iliwafikiria kwanza mawakala wake ili wasipoteze ajira waliyokuwa nayo.

“TARURA imeundwa kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM), na katika vipengele vya ilani hiyo vinasisitiza suala la kuongeza ajira,hivyo sisi kama TARURA hatuwezi kupoteza ajira za hawa vijana ilhali tunafanya kazi ya kutekeleza Ilani hiyo,”anasema Kitogo.

Anasema jambo walilolifanya wakati wanafikiria kuuanza mfumo huo ni kuhamasisha wananchi wakiwemo mawakala hao kutengeneza vikundi kupitia afisa wa maendeleo ya jamii na kusajili kwa mkurugenzi waweze kupata usajili na kufungua akaunti na kisha wanawapa ujuzi mbalimbali.

“Kila mwaka TARURA inakuwa na bajeti ya maboresho ya barabara, na katika kazi ndogo ndogo ambazo sio za kitaalam kama kufyeka barabara, kufagia, kusafisha mitaro tunawapa kazi hizo wafanye wao, hivyo mfumo huo hautakuwa sababu ya wao kupoteza ajira,”anabainisha.

Kitogo anasema wanatarajia kuwepo kwa changamoto wakati wa kuanza matumizi ya mfumo huo lakini wana imani mambo yatakuwa sawa kadri siku zitakavyoenda.

Msimamizi wa mapato na maegesho kutoka TARURA Mwanza Nelson Mfinanga anasema nia ya TARURA ni njema ya kuhakikisha kila pesa inayotolewa kwenye ushuru wa maegesho inafika serikalini.

“Ushuru huu mnaolipa unarudi kwenu wenyewe wananchi kupitia maendeleo mnayoletewa na serikali, ushuru huu mnaotoa utatusaidia kupatikana kwa barabara bora ili muweze kusafirisha mazao yenu na kuongeza uchumi wa Taifa,”anasema Mfinanga.

Afisa Tehama wa TARURA Mwanza Anorld Chao anasema malipo yatalipwa kupitia mitandao ya simu baada ya kupata kumbukumbu namba ya malipo ambayo itapatikana kwa kupiga *152*00# na kufuata maelekezo.

“Ukipiga namba hiyo utafuata maelekezo kwa kuchagua kipengele cha nishati na usafiri, halafu utakuta TARURA e-parking, kulipa maegesho, utaingiza namba ya gari au pikipiki, mkoa ,eneo la maegesho na mwisho unachagua aina ya gari au pikipiki,”anasema Chao.

Anasema ukipata kumbukumbu namba unachagua mwenyewe kulipia kwa mtandao wa simu ulionao.

TARURA imeanzishwa chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Sura ya 245 na kutangazwa rasmi katika Gazeti la Serikali Na. 211 la Mei 12, 2017 na kufunguliwa rasmi Julai 2, 2017 ikiwa na dhamira ya Kupanga, Kusanifu, Kujenga na Kufanya matengenezo ya mtandao wa barabara zake.

Matangazo

  • INVITATION FOR TENDERS - DODOMA June 08, 2022
  • TANGAZO LA KAZI -KAGERA April 21, 2022
  • CALL FOR INTERVIEW - MTWARA January 17, 2022
  • CALL FOR AN INTERVIEW - MWANZA December 23, 2021
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ZIARA YA MTENDAJI MKUU TARURA YALETA FARAJA KWA WANANCHI - KASEKE

    May 19, 2022
  • TARURA TANGANYIKA WAPEWA SIKU 30 KUKAMILISHA UKARABATI DARAJA LA IFUME

    May 18, 2022
  • WATUMISHI TARURA WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    May 16, 2022
  • BODI YA USHAURI TARURA YAFANYA UKAGUZI UJENZI WA BARABARA KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA

    April 29, 2022
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Barua pepe za Watumishi - TARURA
  • Mfumo wa Maegesho (TeRMIS)
  • Lipia Maegesho (TeRMIS)
  • Mfumo wa eMrejesho

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Instragram_tarura
  • twitter_tarura
  • Mfumo wa Maegesho (TeRMIS)
  • Mfumo wa eMrejesho

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),TARURA HOUSE GOVERNMENT CITY -MTUMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa