• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Miradi iliyo kamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyochini ya Ununuzi
    • Project and Program
    • RISE - FEB- 2021
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Huduma na Uendeshaji
    • Kurugenzi ya Barabara za Vijijini
    • Kurugenzi ya Barabara za Mijini
    • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
    • Kitengo cha udhibiti Ubora na Utafiti
    • Sehemu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA)
    • Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu
    • Sehemu ya Mipango
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Waratibu wa Mikoa
    • Mameneja wa Halmashauri

TARURA WILAYANI LIWALE YATEKELEZA MIRADI YA AHADI ZA VIONGOZI

Posted on: December 10th, 2020

TARURA WILAYANI LIWALE YATEKELEZA MIRADI YA AHADI ZA VIONGOZI 

Na. Thereza Chimagu.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, umetekeleza miradi ya Ahadi za Viongozi kwa kukamilisha ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami zenye jumla ya urefu wa Kilomita 0.779.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Mhandisi Livingstone Shija alieleza kuwa utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Viongozi umekamilika kwa asilimia 100 baada ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami ya Wamo-Soko la Zain Km 0.31, Sanabu-Mangota-Mponda Km 0.329 na Mchanda Guest-Ngosha Butcher Km 0.14 kukamilika na kuanza kutumika.

“Hapo awali wananchi walikuwa wanapata shida sana na barabara hizi ikiwemo vumbi, matope na maji kujaa, lakini baada ya utekelezaji wa mradi huu wananchi wameanza kunufaika na barabara hizi na wanaendelea kufanya shughuli zao za maendeleo bila usumbufu wowote”, alisema Mhandisi Shija.    

Mkazi wa Lindi Bw. Silaji Abdallah ameishukuru Serikali kwa kutengeneza barabara hizo kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wa barabara hizo umesaidia kupunguza kero ya vumbi na maji kujaa katika barabara.

‘‘Tunashukuru Serikali kwani barabara ni nzuri na mazingira yanapendeza, pale mwanzoni tulikuwa tunapata usumbufu mkubwa hasa sisi tunaofanya biashara zetu eneo la sokoni kwani kipindi cha mvua maji yalikuwa yanajaa sana kutokana na kutokuwa na mifereji, lakini kwasasa maji yanapita kwenye mifereji na tunafanya biashara zetu kwa raha bila usumbufu, alisema Bw. Abdallah.

Aidha, mbali na utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Viongozi, TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Liwale imetekeleza mradi mwingine wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa mita 546 ambayo imewekewa mitaro na makalavati na pia kuna mpango wa kutekeleza mradi mwingine wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa mita 450.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijni (TARURA) Halmashauri ya Wilaya ya Liwale unaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya matengenezo ya barabara, madaraja na vivuko ili kuongeza shughuli za uzalishaji na kukuza uchumi kwa wananchi wa Wilaya hiyo.

Matangazo

  • INVITATION FOR LOGO DESIGN COMPETITION November 12, 2020
  • SHINDANO LA KUANDAA NEMBO (LOGO) YA TARURA-KISWAHILI November 12, 2020
  • WALIOITWA KWENYE USAILI KADA YA UDEREVA TARURA MKOA WA TANGA November 06, 2020
  • KUITWA KWENYE USAILI-KIGOMA October 30, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MHE. JAFO ARIDHISHWA NA UJENZI WA BARABARA YA UHURU

    March 06, 2021
  • DARAJA LA MWASONGE KUUNGANISHA MISUNGWI NA NYAMAGANA

    February 22, 2021
  • TARURA INAVYOBORESHA MIUNDOMBINU MKOA WA RUVUMA

    February 18, 2021
  • TARURA INAVYOENDELEA KUTATUA KERO KWA WANANCHI MKOANI DODOMA

    February 03, 2021
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Tarura Barua pepe za Watumishi

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Instragram_tarura
  • twitter_tarura

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),TARURA HOUSE GOVERNMENT CITY -MTUMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa