• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
      • Bodi ya Ushauri
      • Uongozi wa Wakala
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Project and Program
    • RISE - MAY- 2021
    • TeRMIS
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Barabara
      • Sehemu ya Barabara Vijijini
      • Sehemu ya Barabara Mijini
    • Kurugenzi ya Mipango na Miundombinu
      • Sehemu ya Usalama Barabarani
      • Sehemu ya Mipango na Miundombinu ya Barabara
    • Kurugenzi ya Huduma Saidizi
      • Sehemu ya Rasilimali Watu na Utawala
      • Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini
    • Kitengo cha Uhasibu
    • Kitengo cha Tafiti na Udhibiti Ubora
    • Kitengo cha Teknlojia ya Habari na Takwimu
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Ununuzi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
    • Kitengo cha Mazingira na Maendeleo ya Jamii
    • Ofisi ya Mkoa
    • Ofisi ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Mameneja wa Mikoa
    • Mameneja wa Wilaya

TARURA YAENDELEA KUFUNGUA BARABARA MAFIA

Posted on: January 26th, 2022

TARURA YAENDELEA KUFUNGUA BARABARA MAFIA

Na. Geofrey A. Kazaula, Mafia.

Wakala wa Barabara za Viijini na Mijini (TARURA) umeendelea kufungua barabara ili kuwezesha wananchi kufika kusiko fikika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Mafia, Mhandisi Francis Mugisha ameeleza kuwa katika mwaka wa Fedha 2021/22 Wilaya ya Mafia imetengewa bajeti ya Shilingi  765,580,000  kutoka Mfuko wa Barabara kwa ajili ya matengenezo ya barabara, fedha za miradi ya maendeleo Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na Shilingi Bilioni 1 fedha zilizotokana na tozo mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Mhandisi Mugisha alisema kuwa moja ya kazi zinazoendelea katika Wlaya ya Mafia ni pamoja na kuiongezea upana barabara ya Ndagoni-Kitimondo yenye urefu wa Kilomita 10 na kuipandisha hadhi kutoka kiwango cha udongo kwenda kiwango cha changarawe ili kuwezesha wakulima kusafirisha mazao yao hadi sokoni.

‘‘Wananchi wameridhia kuondoa mazao yao bila fidia ili kuweza kuipandisha hadhi barabara hii ambayo ni tegemeo kwao kwa ajili ya kusafirisha mazao kufika sokoni”, alisema Mhandisi Mugisha.

Naye Mkazi wa Mafia, Bw. Khamis Habibu alieleza kuwa lengo la wananchi kukubali kuondoa mazao yao ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo ni kumaliza kilio cha muda mrefu cha ukosefu wa barabara huku akiipongeza Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo na kuwatengea fedha.

‘‘Hapa ni kisiwani na kilio cha barabara kimekuwa cha muda mrefu lakini sasa serikali imelitambua hilo na hivyo tumeridhia mazao yetu yaondolewe maana maendeleo hayawezekeni bila barabara”, alisema Bw. Habibu

Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Mhandisi Martin Ntemo ameelezea kuwa Wilaya ya Mafia imekua na changamoto ya barabara kwa muda mrefu lakini baada ya kuanzishwa kwa TARURA tayari barabara nyingi zimeanza kufunguliwa na kwamba ujenzi wa barabara ya lami Mafia mjini umeanza ambapo kukamilika kwa barabara hiyo kutachochea shughuli za kiuchumi na utalii.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI -KAGERA April 21, 2022
  • CALL FOR INTERVIEW - MTWARA January 17, 2022
  • CALL FOR AN INTERVIEW - MWANZA December 23, 2021
  • TANGAZO LA KAZI -MWANZA December 10, 2021
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ZIARA YA MTENDAJI MKUU TARURA YALETA FARAJA KWA WANANCHI - KASEKE

    May 19, 2022
  • TARURA TANGANYIKA WAPEWA SIKU 30 KUKAMILISHA UKARABATI DARAJA LA IFUME

    May 18, 2022
  • WATUMISHI TARURA WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    May 16, 2022
  • BODI YA USHAURI TARURA YAFANYA UKAGUZI UJENZI WA BARABARA KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA

    April 29, 2022
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Barua pepe za Watumishi - TARURA
  • Mfumo wa Maegesho (TeRMIS)
  • Lipia Maegesho (TeRMIS)
  • Mfumo wa eMrejesho

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Instragram_tarura
  • twitter_tarura
  • Mfumo wa Maegesho (TeRMIS)
  • Mfumo wa eMrejesho

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),TARURA HOUSE GOVERNMENT CITY -MTUMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa