• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA
Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
  • Miradi na Programu
    • Project and Program
    • RISE - MAY- 2021
    • TeRMIS
  • Utawala
    • Kurugenzi ya Barabara
      • Sehemu ya Barabara Vijijini
      • Sehemu ya Barabara Mijini
    • Kurugenzi ya Mipango na Miundombinu
      • Sehemu ya Usalama Barabarani
      • Sehemu ya Mipango na Miundombinu ya Barabara
    • Kurugenzi ya Huduma Saidizi
      • Sehemu ya Rasilimali Watu na Utawala
      • Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini
    • Kitengo cha Uhasibu
    • Kitengo cha Tafiti na Udhibiti Ubora
    • Kitengo cha Teknlojia ya Habari na Takwimu
    • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
    • Kitengo cha Ununuzi
    • Kitengo cha Huduma za Sheria
    • Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
    • Kitengo cha Mazingira na Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu Mbalimbali
    • Majarida
    • Vipeperushi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Maktaba ya Picha
  • Manunuzi
    • Taarifa ya Manunuzi
    • Zabuni za Wazi
    • Tuzo za Zabuni
  • Mitandao ya Barabara
    • Mitandao ya Barabara za Tarura
  • Mikoa
    • Mameneja wa Mikoa
    • Mameneja wa Wilaya

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA WAANZA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA MALIPO YA USHURU WA MAEGESHO (TARURA e-PARKING)

Posted on: May 2nd, 2019

Wakazi wa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela tarehe 02/05/2019 wameanza rasmi kutumia mfumo mpya wa Kielektroniki wa malipo ya ushuru wa maegesho (TARURA e-PARKING) ambao unatumia mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya serikali yaani Government Electronic Payment Gateway (GePG).

Baada ya serikali kutoa maagizo kwa taasisi za serikali kuhakikisha ifikapo Juni mwaka huu ziwe zimeshajiunga kwenye mfumo wa malipo wa serikali kwa njia za kielektroniki (GePG) ili kutimiza matakwa ya sheria ya Fedha za Umma Sura ya 348, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umezindua mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya ushuru wa maegesho kwa vyombo vya usafiri na moto (TARURA e-Parking) kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.

Lengo la TARURA kutumia mfumo wa Kielektroniki ni kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya serikali ili kuboresha miundombinu ya barabara za vijijini na mijini.

Mfumo huu (TARURA e-PARKING) ni rahisi na salama ambapo mtumiaji wa maegesho yaliyo kwenye hifadhi ya barabara za TARURA anapaswa kulipia maegesho kwa kutumia simu yake ya mkononi, benki au wakala na pesa atakayolipa inakwenda moja kwa moja kwenye akaunti ya serikali.

Faida ya kuanzisha na kutumia mfumo huu utampunguzia mtumiaji wa maegesho kero ya kudaiwa ushuru wa maegesho na kufungiwa chombo chake cheni, kwani mtumiaji atalipa mwenyewe kwa kutumia simu yake ya mkononi, wakala au benki. Pia faida nyingine utasaidia kuboresha mipango ya barabara na kupunguza changamoto za maegesho yaani “parking”.

Malipo yanafanyika kwa njia mbili; Kwanza unatakiwa upate kumbukumbu namba ya malipo ambayo utaipata kwa kubonyeza *152*00# kisha fuata maelekezo. Utachagua namba 4 (Nishati na Usafiri), utachagua namba 2 (TARURA e-Parking), utachagua namba 1 (kulipia maegesho), Ingiza namba ya chombo, chagua mkoa, chagua eneo la maegesho, chagua aina ya chombo. Kisha utapokea ujumbe mfupi wenye kumbukumbu namba na kiasi unachotakiwa kulipia maegesho.

Hatua ya pili baada ya kupata kumbukumbu namba (control number) unalipia maegesho kwa kutumia mitandao yote ya simu T-Pesa, M-Pesa, Airtel Money, Tigopesa, Halopesa, Ezypesa unalipa kwa wakala yoyote au kwa kutumia tawi lolote la benki.

Ukitaka kujua unadaiwa maegesho bonyeza *152*00# kisha fuata maelekezo. Utachagua namba 4 (Nishati na Usafiri), utachagua namba 2 (TARURA e-Parking), utachagua namba 2(angalia deni).

Malipo ya maegesho ni kwa siku lipia maegesho kabla ya saa sita usiku, lipia maegesho kuepeuka faini isiyo ya lazima.

Mkazi wa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemelea sasa malipo ya maegesho ni kiganjani mwako.

Imetolewa na:

Bebi Kapenya

PRO-TARURA

 

Matangazo

  • INVITATION FOR TENDERS - DODOMA June 08, 2022
  • TANGAZO LA KAZI -KAGERA April 21, 2022
  • CALL FOR INTERVIEW - MTWARA January 17, 2022
  • CALL FOR AN INTERVIEW - MWANZA December 23, 2021
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ZIARA YA MTENDAJI MKUU TARURA YALETA FARAJA KWA WANANCHI - KASEKE

    May 19, 2022
  • TARURA TANGANYIKA WAPEWA SIKU 30 KUKAMILISHA UKARABATI DARAJA LA IFUME

    May 18, 2022
  • WATUMISHI TARURA WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    May 16, 2022
  • BODI YA USHAURI TARURA YAFANYA UKAGUZI UJENZI WA BARABARA KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA

    April 29, 2022
  • Angalia zote

Video

Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Barua pepe za Watumishi - TARURA
  • Mfumo wa Maegesho (TeRMIS)
  • Lipia Maegesho (TeRMIS)
  • Mfumo wa eMrejesho

Tovuti Muhimu

  • Wakala wa Barabara
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • OR-TAMISEMI
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano
  • Utumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Baraza la Mitihani
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Instragram_tarura
  • twitter_tarura
  • Mfumo wa Maegesho (TeRMIS)
  • Mfumo wa eMrejesho

Waliotembelea duniani

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    TANZANIA RURAL AND URBAN ROADS AGENCY (TARURA),TARURA HOUSE GOVERNMENT CITY -MTUMBA

    Anuani ya Posta: P.O BOX 11042, DODOMA

    Simu ya mezani: 026-2963846

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ceo@tarura.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

StatCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hati Miliki @2017 TARURA. Haki zote zimehifadhiwa